Jumamosi , 9th Jan , 2016

Umati wa watanzania wakiwepo wasanii maarufu wa maigizo na muziki wamejitokeza usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar kumpokea kwa shangwe mwanasoka Mbwana Samatta baada ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Dokii akiongea na EATV

eNewz kutoka eneo la tukio, tumekutana na baadhi yao, akiwepo nguli wa taarab Mzee Yusuph aliyechukua nafasi hiyo kumtaka Samatta asibweteke na aendelee kufanya jitihada, akiwepo pia Dokii ambaye sambamba na furaha ya ujio wa Samatta ametoa pia kionjo cha live cha rekodi aliyomtengenezea nyota huyo baada ya ushindi.

Wasanii hao wamesema kuwa, hawakuweza kukosa kuhudhuria mapokezi hayo kutokana na ukweli kuwa hatua ya mafanikio ya Samatta ni kubwa na ya kihistoria inayoijengea nchi ya Tanzania heshima kubwa nje ya mipaka yake, na pia kutoa hamasa kwa wanasoka na wadau kwa ndani juu ya maendeleo ya mchezo huo.