Matonya ahamia Kenya, kumiliki hoteli na kiwanda

Jumamosi , 23rd Mei , 2020

Mkali wa kitambo katika Bongo Fleva, Matonya amefunguka mengi juu ya maisha yake hivi sasa pamoja na mipango yake katika uwekezaji nje ya muziki anaoufanya.

Msanii Matonya

Akiwa katika Friday Night Live (FNL) Matonya amesema kuwa hivi sasa amehamishia maisha yake nchini Kenya ambako alianza kuishi tangu mwaka 2010, huku akiweka wazi baadhi ya miradi yake anayoifanya hivi sasa.

"Kwa sasa ninaishi sana Kenya ambako naishi na ndugu zangu wawili nikiwa na miradi yangu, mke wangu hayupo kule kwa sababu sitaki kumuweka katikati kwenye kazi zangu. Nilianza kuishi Kenya tangu miaka 10 iliyopita kwahiyo nashukuru Mungu maisha yanasonga", amesema Matonya.

"Mama yangu mzazi ambaye yuko Tanga amejaribu kujenga hoteli yenye vyumba 15 self container ambayo watu watalala juu na chini, mimi nilikuwa najenga ila mama amenizuia. Mpango wa pili tunapigania kujenga kiwanda cha mabati huko Mapinga, Bagamoyo lakini Mungu akipenda nitakuja kuongelea rasmi", ameongeza Matonya.