Alhamisi , 19th Sep , 2019

Mbunge wa Segerea Bonnah Kamoli amesema anavutiwa sana na Msanii wa Muziki wa Bongofleva nchini Alikiba kutokana na ngoma zake, huku akikiri Msanii huyo ni mpiga kura wake.

Bonnah Kamoli ametoa kauli hiyo katika katika kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kila siku ya Jumatano kupitia kurasa wa Facebook na YouTube ya East Africa TV, ambapo alitakiwa kuchagua Msanii mmoja kati ya Alikina au Marioo.

"Unajua Alikiba ni mpiga kura wangu, ukinambia nichague moja, kati ya Alikiba na Marioo nitamchagua Alikiba kwanza ni msanii mzuri na amekaa kwenye game kwa muda mrefu sana, unajua kwenye kazi zao hizi kukaa kwenye muda mrefu ni kazi sana." amesema Mbunge Bonnah Kamoli.

Awali Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi Bonnah Kamoli, amesema yeye anaweza kugombea nafasi ya juu zaidi ifikapo Uchaguzi wa 2025 na ule wa 2030.

Tazama mahojiano kamili hapo chini.