Alhamisi , 14th Mei , 2015

Jeff Kiwa, mdau mkubwa na meneja mwenye rekodi ya kufanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa nchini Uganda, amejipanga kuachana na shughuli hiyo ya umeneja na kufanya mambo mengine baada ya kuchafuliwa jina lake katika kazi hiyo.

meneja wa wasanii wa muziki nchini Uganda Jeff Kiwanuka

Jeff amepata msukumo mkubwa wa kuchukua hatua hiyo, hasa baada ya kutupiwa lawama kuhusu kifo cha msanii AK47, na pia skendo ya kutumia vibaya pesa za Radio pamoja na Weasel, kipindi wakifanya kazi pamoja kati ya mambo mengine.

Kwa mujibu wa taarifa, Jeff kwa sasa ameamua kukabidhi majukumu yake yote yanayohusiana na muziki kwa mdogo wake ambaye anafahamika kwa jina Allan Kiwanuka.