Alhamisi , 22nd Feb , 2018

Meneja wa wasanii ambaye ametoa wasanii wengi bongo, Papa Misifa, ameitaka serikali kutoweka sheria kali kwa wasanii na mameneja wao, kwani itawagharaimu vijana hao ambao kwa namna moja au nyingine wanajaribu kujikwamua kiuchumi.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Papaa Misifa amesema wasanii wengi bado hawajajielewa hivyo wakiweka sheria kali itawafanya washindwe kufanya kazi nao, na kusababisha wasanii kuingia mtaani kufanya uhalifu.

Sheria mkiweka wasanii watazidi kuiba mapikipiki ya watu, waachieni watu waingize hela zao zipotee, zikishatoka kama zimepotea bure basi zimeondoka, kwa sababu hakuna msanii ambaye anajielewa mpaka sasa na ndio maana bado wanakaa na mameneja wao mpaka leo, hawana heshima, hawataweza”, amesema Papaa Misifa.

Papaa Misifa ni miongoni mwa mameneja ambaoi wako vizuri kipesa na ameshatoa wasanii wakubwa bongo kama Sam wa ukweli, Richi Mavoko na wengine wenye majina makubwa kwa sasa.