
Msanii Mwijaku
Mwijaku amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, na kusema mlinzi aliyekuwa naye amepitia katika mafunzo ya kijeshi na hajawahi kucheka tangu amekuwa naye.
"Unajua kuna umri na mafanikio ukishayafikia, jinsi ya ukubwa wangu, jina langu lilivyo na brand yangu imeshakuwa kubwa, kwa hiyo nimeombwa nisitembee peke yangu, kwa hiyo huyu ni "bodyguard" wangu ambaye ana mafunzo ya kijeshi na kwenye mizunguko yangu mingi huwa natoka naye" ameeleza Mwijaku.
"Nipo naye kwa sababu ya ulinzi ukitaka kunishambulia mimi mtamjua, maana huyu haijui raha yoyote mjini, anachojua mimi nitoke na nirudi nyumbani salama, na amefunzwa kutulinda watu kama sisi, hata mimi sijawahi kumuona akicheka hata siku moja na nipo kwa wiki ya tatu sasa" ameongeza.
Moja kati ya habari iliyozua gumzo na kuongelewa sana kwa mwaka huu 2019, ni juu ya wasanii kutembea na walinzi "Bodyguard".