
Mo Cheddah
Mo Cheddah amesema kuwa, amekuwa akifanya muziki tangu akiwa na miaka 12, na muda wote huo muziki umekuwa ni sehemu ya maisha yake hadi kufikia wakati ambapo aliona uhitaji wa kujihusisha na mambo mengine kwanza.
Mo Cheddah ameweka wazi kuwa, katika muda wote nje ya muziki amekuwa akijifunza mambo mbalimbali na kujionea jinsi muziki unavyokwenda, na kwa kutumia kipaji chake amejipanga kuwashangaza mashabiki kwa ujio mpya.