Jumatatu , 27th Apr , 2015

Waimbaji mahiri kutoka nchini Kenya, mapacha watatu ambao wanafahamika kwa jina Moipei Sisters wamepata nafasi ya kuimba wimbo wa Taifa wa Marekani katika mechi ya mpira wa kikapu ya San Antonio Spurs dhidi ya LA Clippers siku ya Jumapili.

waimabji wa kundi la Moipei Sisters wa nchini Kenya

Nafasi hiyo kwa Moipei Sisters ambao kwa sasa wapo nchini Marekani kimasomo, imekuwa ni jukwaa lingine kubwa kuwawezesha kuonyesha uwezo na vipaji vyao vikubwa katika kuimba , na kupeperusha bendera ya nchi yao.

Moipei Sisters ambao pia walifanya vizuri sana kuimba katika shughuli za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta, kupitia nafasi hiyo wameweka ujumbe kwa mashabiki wao katika mtando, kuwataka kufahamu kuwa, kila ndoto inawezekana kutimia pale inapowekewa malengo.