Jumamosi , 23rd Jan , 2016

Producer Mona Gangster ametetea uwezo wake wa kumsimamisha msanii mpya na kumfikisha katika ngazi ya mafanikio kama ilivyokuwa kwa Young Killer, ikionekana kuwa jitihada zake za kumuingiza msanii wake mpya Motra katika ramani zinasuasua.

Mona Gangster

Mona Gangsta amewataka mashabiki wa muziki kumpatia mwaka huu ili kuwadhihirishia kuwa ana uwezo wa kutengeneza kipaji, akizungumzia pia sababu za kuchelewa kwa video ya msanii wake huyo kupitia mahojiano tuliyofanya naye hapa.