Jumanne , 17th Jun , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Moze Radio ametajwa kama moja kati ya mastaa ambao wamewekeza nguvu za pekee kusaidia ndugu zao kwa kiasi kikubwa kutokana na kipato ambacho wamejitengenezea kutoka katika sanaa ya muziki.

Msanii wa muziki Moze Radio

Tofauti na mastaa wengine, Moze Radio ameweza kujitoa kuwaendeleza ndugu zake na kufungua miradi mbalimbali katika kijiji anachotoka, ili kuhakikisha kuwa anawaendeleza kuwatoa katika umasikini.

Radio katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni amesema kuwa, ndugu zake ndio kitu cha kwanza kabisa kwake, na kuwa vyombo vya habari vinaweza kuandika chochote kumhusu na akachukulia poa, ila si katika suala la kumuandika vibaya ndugu yake yoyote.