Alhamisi , 12th Nov , 2020

Katika post 3 kati ya 5 za mwisho alizoweka kwenye ukarasa wake wa Instagram msanii na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule 'Prof Jay' ameweka maneno ambayo yanatia nguvu na kutokata tamaa baada ya matokeo ya Uchaguzi kutangazwa wiki mbili zilizopita.

Kulia ni Joseph Haule "Prof Jay" na kushoto ni Joseph Mbilinyi "Mr II Sugu"

Sasa tukirudi kwenye post ya leo ambayo ameweka muda mfupi uliopita Prof Jay ameandika kuwa "Ishi ulaumiwe, kufa usifiwe hiyo ndiyo hulka ya binaadam

Baada ya kuandika hivyo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini  Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II Sugu akamtania kwa ku-comment kuwa "Mbunge aliyeporwa uchaguzi" .

Prof Jay na Mr II Sugu ni wasanii ambao wameingia kwenye siasa na kuwa Wabunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wote hawakubatika kuendelea kuwatumikia wananchi wao baada kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika siku ya Oktoba 28.