Msanii aeleza alivyopotezwa na wapenda Kiki

Jumamosi , 6th Jul , 2019

Msanii wa kike aliyetamba na ngoma yake ya "Nimempata" Pamela Dafa maarufu kama Pam D, amefunguka kuwa watanzania wanapenda kuwaangalia watu wenye kiki.

Pam D

Pam D amesema hayo kwenye show ya Friday Night Live "FNL" ya East Africa Television, baada ya kuulizwa ni kitu gani kilichokwamisha maendeleo yake ya kimaisha na kimuziki.

"Kimuziki cha kwanza ni kutokuwa na uongozi na watu wa kunisimamia, vitu ni vingi kama kutafuta 'connection' ni vitu ambavyo vimechangia sana'', amefunguka.

Pam D ameongeza kuwa ''kingine unajua watanzania wanapenda kuwaangalia watu wenye kiki sana, sasa mimi sio mtu wa kiki nipo poa tu, watu wanataka matukio mimi sio mtu wa matukio."

Kwa sasa Pam D ameachia kazi yake mpya ya audio na video iitwayo Kizunguzungu, aliyomshirikisha msanii Foby.