Msanii atangaza kugombea Urais Marekani

Ijumaa , 5th Jul , 2019

Msanii wa hip hop asiyeishiwa na vituko nchini marekani, Young Thug, ametangaza nia yake ya kutaka kugombea uraisi wa nchi hiyo ifikapo mwaka 2024.

Young Thug

Rapa huyo ametangaza uamuzi wake baada kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, ambapo amesema,"nina nia ya kugombea Urais 2024, Gunna atakuwa makamu wangu wa Rais".

Aidha rapa huyo amewahi kuzua kituko kwa kutangaza kujiita jina la 'Sex', kutokana na kupendelea kuvaa nguo za kike.

Msanii mwingine aliewahi kutangaza nia ya kuwa raisi ni rapa Kanye West, kutokana na kuwa karibu na Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump.