Jumatano , 20th Nov , 2019

Muigizaji wa BongoMovie Shamsa Ford, amesema anaweza kumpiga mtu vibao endapo kama atamwambia kwamba hali ya maisha ya sasa ni ngumu, kwa sababu yeye bado anaingiza pesa na haoni ugumu huo wa maisha.

Muigizaji Shamsa Ford

Shamsa Ford amesema hivyo kupitia EATV & EA Radio Digital,  baada ya kuulizwa ni jambo gani ambalo  hawezi kuamini endapo ataambiwa na mtu yeyote.

"Jambo ambalo siwezi kuliamini kabisa ni pale  ukiniambia hali  ngumu nakukatalia, kwa sababu ninachokiona sasa hivi hali sio ngumu ukifanya kazi pesa zipo, ila kwa wale wanaopenda njia fupi, wanaojipatia pesa kwa njia ambayo siyo sahihi au rahisi ndiyo wanaona hali ni ngumu" amesema.

"Lakini mbona nikikaa dukani na kupambana naona pesa zinakuwepo, ukiniambia hali ni ngumu naweza kukupiga hata vibao ni uongo tu, labda wanasema hali ngumu kwa sababu wanashinda nyumbani hawataki kwenda kutafuta ila kama unatoka kutafuta hali siyo ngumu kabisa" ameongeza.