Jumanne , 22nd Dec , 2015

Meneja wa star wa muziki Ommy Dimpoz, Mubenga ameeleza kuwa anatamani uwekezaji mkubwa wa pesa ambazo wasanii wanaufanya katika video nnje ya nchi kwa sasa urejee hapa nyumbani, kukiwa na haja ya mamlaka husika kuweka mazingira mazuri kwa wasanii.

Mubenga

Mubenga ambaye kwa sasa yupo katika shughuli ya kusambaza video mpya ya Ommy Dimpoz, Achia Body aliyoifanyia nchini Afrika Kusini amesema hayo akitolea mfano wa video ya kwanza ya Ommy Dimpoz - Nai Nai kupelekea moja ya watu aliowasaidia eneo la kufanyia video kupoteza kazi yake kwa kitendo hicho.

Tags: