Picha ya Mwana FA akiwa na msanii Mac Voice
Mwana FA amesema Serikali imeanza kuchukua hatua za kulifuatilia sakata hilo ili kupata ukweli wa madai yaliyotolewa na pande husika, huku akiahidi kuwa suala hilo litafanyiwa kazi kwa haraka ili kupatikana suluhisho la haki kwa wahusika.
Pia amefafanua kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha haki na maslahi ya wasanii yanazingatiwa, huku akisisitiza umuhimu wa mikataba iliyo wazi na inayolinda pande zote katika sekta ya sanaa.





