Alhamisi , 8th Mei , 2014

Rapa anayeiwakilisha poa game ya muziki kwa miaka mingi hapa Bongo, Mwana FA ambaye mbali na usanii, ni msomi mwenye shahada ya uzamili, amesisitiza kuwa, ili muziki wetu uzidi kufika mbali, ni muhimu kwa wasanii pia kuzingatia suala la elimu.

Mwana FA

MwanaFA amesema kuwa, ingawa mawazo ya watu wengi yamejengeka katika kwenda shule ili kupata cheti na kuajiriwa, kuna haja ya kubadilisha mtazamo hususan kwa wasanii kwenda shule kwa lengo la kupanua mawazo, ili kuleta maana zaidi katika kazi zao na namna ya kushughulikia mambo yao na kusimamia kazi zao.

Mana FA, aka. Tiger Woods wa Rap Bongo, aka The ChoirMaster, amesisitiza kuwa, wasanii wakisoma, kutatokea mabadiliko makubwa yenye manufaa kwa mashabiki kupitia kazi watakazotengeneza.