Alhamisi , 6th Oct , 2022

Msanii wa filamu Tausi Mdegela (Rais wa Watoto) ameshea ujumbe kuhusu wakina mama wanaolea watoto wenyewe (Single mother's) kwa kuwahimiza kuwapambania watoto na hata mzazi mwenza hatoi huduma.

Picha ya msanii wa filamu Tausi Mdegela, mtoto wake na baba wa mtoto wake

Akishea ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Instagram Tausi ameandika kwamba 

"Single mother tujifunze hii sana hata kama hatoi huduma baki na mtoto wako mpambanie. Mimi Pipina wangu nampambania mwenyewe na maisha yanaendelea, Mungu endelea kunipa nguvu kwako kila kitu kinawezekana".

Tausi Mdegela amepata mtoto wake wa kwanza wa kike mwanzoni mwa mwaka 2020 na mpenzi wake Chriss.