Wini adai kutongozwa kwake ni baraka

Ijumaa , 8th Nov , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Wini Tz, amefunguka na kusema kwa sasa yupo single ila anaona  baraka sana kutongozwa na haoni kama ni jambo kubwa sana, pale anapofuatwa na wanaume.

Wini Tz ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kwa siku huwa anatongozwa na wanaume wangapi.

"Kutongozwa ni kawaida hamna kitu ninachohisi, huwa nasikiliza tu halafu naendelea na mambo yangu, sioni kama ni jambo kubwa kunitongoza, ila kwa sasa hivi nipo single," amesema Wini Tz.

Aidha WiniTz ameongeza kuwa, "Pia kutongozwa ni sehemu ya baraka, kuna watu wanatembea hata hawatongozwi wala hawasalimiwi, kwangu mimi naona poa tu kama wananijaribu ila naamua hapohapo kusema ndiyo au hapana".