Mwanaume asiye na pesa,wanini sasa? - Gigy Money

Jumatatu , 10th Feb , 2020

Mrembo Gigy Money, amekiri kusema ni kweli  yupo  katika penzi na mnaijeria Hunchy Huncho kwa ajili ya pesa, kwa sababu mapenzi bila pesa unaweza ukamsaliti mwenza wako.

Picha ya msanii Gigy Money

Gigy Money ameiambia EATV & EA Radio Digital, kuwa ameshapitia sana mahusiano ambayo mwanaume hana pesa, kilichotokea ni kugombana na kudharauriana.

"Ni kweli nipo kwake kwa ajili ya pesa na anaendelea kunipa, mapenzi bila pesa unakuwa unamsaliti mwanaume wako, ila akiwa anakupa kila kitu kama raha za dunia, kukupa mahitaji na anakupa pesa kwanini usitulie, na kwa mwanaume ambaye hana pesa mimi wa nini sasa hivi" amesema Gigy Money

Aidha Gigy Money ameendelea kusema "Najituma usiku kucha silali nahangaika klabu ili nipate kitu nipeleke nyumbani, kwa hiyo mwanaume ambaye hana pesa tutagombana na kudharauliana tu, bora anipe mawazo ila pesa yake iwe imetumika, nimeshatumika sana kwa mwanaume asiyekuwa na pesa hadi nimechoka waache wenye hela" ameongeza

Gigy Money kwa sasa amerudiana na mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria Hunchy Huncho, baada ya kutengana kwa kipindi cha muda mfupi.