Jumanne , 21st Jun , 2016

Baadhi ya wadau wanao fatilia muziki wa Bongo fleva nchini wanasema ubunifu mkubwa uliofanyika katika kuandaa video ya ngoma 'Jike Shupa' ilikuwa Nuh Mziwanda apotee kabisa na kufa kifo cha mende na muziki wake umepata nguvu baada ya video hiyo.

Nuh Mziwanda

Wengi wanasema video ya 'Jike Shupa' ndiyo imemsaidia Nuh na kumfanya atembee kifua mbele kama kapigwa ngumi ya mgongoni, na kuweza kumpatia shoo nyingi ambazo zimezidi kumpa kiki hapa mjini na maisha yake kuonekana yakienda poa tu kama hapo zamani.

Hata hivyo Nuhu amekanusha kuhusiana na watu wanaosema kwamba wimbo wake huo umetungwa na Ali Kiba msanii aliyemshirikisha kwenye korasi na kusema Ali Kiba yeye aliongeza neno Jike Shupa badala ya neno inauma alilokuwa kaliweka Nuh Mziwanda.

Hata hivyo Nuh ameendelea kutamba kwamba yeye ni mwanamuziki habahatishi hivyo mashabiki wake wategemee kupata nyimbo nyingi na zenye ujumbe wa kutosha kwa kuwa yeye anatambua ni kitu gani mashabiki zake wanataka.