Nabii Mashimo atoa ujumbe kwa Mbowe

Ijumaa , 4th Oct , 2019

Mchungaji wa Taifa Nabii Mashimo, ametoa utabiri kwa majimbo yanayoongozwa na wabunge akiwemo Freeman Mbowe,Godbless Lema,Joseph Mbilinyi maarufu Sugu pamoja na Zitto Kabwe, kwamba watakosa ubunge kwenye Uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Akitoa maono hayo ya utabiri, ambayo anadai ameoteshwa na Mungu wake, Mashimo ameanza kumshukuru na kumtia moyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kazi uliotukuka na kuwatetea watanzania walio wanyonge.

Mungu amenionyesha majimbo ya Ubunge ambayo yatapotea mwaka 2020, Jimbo la kwanza ni Arusha Mjini, ambalo linaongozwa na Godbless Lema, Pili ni Mh. Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya Mjini, Tatu ni mwenyekiti wa chama cha Chadema Mh. Freeman Mbowe ambaye anaongoza Jimbo la Hai , mwisho ni Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Mjini” amesema Mashimo.

Nabii Mashimo ameongeza kuwa kama wabunge hao watataka kushinda nafasi zao za uwakilishi wa wananchi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, amesema suluhisho pekee ni wao kutubu na kuokoka.