Nandy na Billnass wawekwa hadharani

Jumatatu , 17th Feb , 2020

Moja ya stori ambayo ilikuwa inatrend katika mitando ya kijamii ni kuhusu msanii Dogo Janja kumtaka Billnass ampost Nandy siku ya wapendanao yaani Valentine Day na asiogope kulinda brand.

Picha ya Billnass na Nandy

Ishu hiyo imekuja baada ya Dogo Janja kumpost mpenzi wake Queen Linna, siku hiyo ya wapendanao ikiwa imepita siku kadhaa tangu kumvisha pete ya uchumba, ambapo Billnass aka-comment kuwa  "Kaka nilikuwa sijui kumbe unakipaji cha kuandika proposals nzuri kabisa ya kukopea hela benki na tukachukua pesa bila riba, sio kwa sound hizi utakuwa umekodi majeshi".

Baada ya comment hiyo ya Billnass, Dogo Janja akajibu kwa kuandika "Mpost kivuruge wewe, acha kuuwa soo,mambo ya kulinda brand Nandy mimi sikubaliii leo".

Sasa kupitia kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, leo Februari 17, 2020, Billnass na Nandy wamejibu tuhuma hizo za kuogopa kupostiana kwenye mitandaoni kisa kulinda brand zao.

"Sio kama siwezi kumpost mpenzi wangu kwa sababu ya kulinda brand hapana, sikuwa na sababu yoyote ya kumpost Nandy kwa sababu sio mpenzi wangu na sipo kwenye mahusiano naye" amesema Billnass.

Aidha kwa upande wa Nandy amesema yeye na Billnass ni marafiki wa karibu ila hawapo kwenye mahu