"Napenda wanaume, Prof Jay kabla ya Chidi"-Mwasiti

Jumatatu , 20th Jul , 2020

Miaka 12 iliyopita Mwasiti alitoa wimbo wa Hao ambao alimshirikisha Chidi Benz, leo ametupa stori iliyopo nyuma ya pazia kwa kusema mipango ilikuwa ni kumshirikisha Prof Jay ila ikashindikana ndipo akatafutwa Chidi Benz.

Kushoto kwenye picha ni Mwasiti, upande wa kulia ni Chidi Benz

"Sikutegemea ule wimbo kama utafanya vizuri kwa sababu ulikataliwa redioni, Producer Lamar aliniomba niimbe kwenye beat lake, nikasema namuhitaji mwanaume, mtu wa kwanza kumuomba alikuwa ni Prof Jay ila akawa bize ikashindikana ndipo nikampata Chidi Benz tena kwa kipindi kile alikuwa wa moto sana" ameeleza Mwasiti

Aidha Mwasiti ameeleza kwa nini hufanya kazi zaidi na wasanii wa kiume kuliko wasanii wa kike kwa kusema  "Watoto wa kiume wapo serios sana unapofanya nao kazi, hawawezi kukuangusha unapofanya nao kazi napenda sana watoto wa kiume kwa sababu hiyo, pili mimi napenda sana HipHop".

Tayari Mwasiti ameshafanya kazi na wasanii wa kiume kama Chidi Benz, Ally Nipishe, Godzilla, Roma, Billnass na G Nako Warawara.