"Nataka kununua ndege" – Tausi

Jumatano , 14th Feb , 2018

Msanii wa filamu bongo ambaye ni mchekeshaji maarufu, Tausi Mdegela, ameweka wazi malengo yake ya kununua ndege ili kusaidia wakazi wa mkoa wa kwao Iringa.

Akizungumza alipokuwa kwenye kipengele cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Tausi amesema kwa sasa anafanya kazi kwa bidii ili apate pesa ya kununua ndege na kuipeleka kwao Iringa, kwani mikoa yote Tanzania ina ndege kasoro Iringa.

"Sasa hivi nafanya kazi napambana, lazima niendeshe ndege iwe isiwe, kila mkoa una ndege kasoro kwetu Iringa, mimi ndio nitanunua, nitakuwa wa kwanza kununua na ntabeba mpaka mbwa", amesema Tausi.

Tausi ni minogoni mwa wasanii wachache wa kipekee Tanzania waliojipatia umaarufu kupitia kazi zao za sanaa, na kupendwa sana na watoto.

 

 

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.