'Naweza kumpata mwanamke yeyote nitakaye' - Marioo

Jumanne , 3rd Dec , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini , maarufu kwa jina la Marioo, amesema kwa sasa alipofikia, pamoja na kazi nzuri anazozifanya anao uwezo wa kumpata na kummiliki mwanamke yeyote anayemtaka.

Pichani ni msanii Marioo 'Toto Bad'.

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Marioo amesema hakuna mtu anayeweza kupenda kazi zako kama hakupendi na wewe , pia kuwa na mwanamke ni muhimu ambapo hadi sasa hajafikiria aina ya mwanamke atakayekuwa naye.

"Sizingatii sana 'bebe', kwa sasa hivi naangalia muendelezo wangu uweje, maana wanawake wapo tu kama unakuwa unafanya kazi nzuri hakuna mtu atakayekuchukia na kutokukupenda, naamini kwenye kazi nzuri nitampata bebe yeyote ambayo natamani kuwa naye hata kama sio leo kesho, au kesho kutwa" ameeleza Marioo.

Pia Marioo amesema kwenye nyimbo zake anazoimba, hakuna jambo lolote ambalo linamuhusu au lililowahi kumtokea, ila huwa anajaribu kufikiria na kuwaza mtaani kinatokea nini au kipi watu wanapenda kusikia kwa wakati huo.