Alhamisi , 17th Jan , 2019

Rapa anayefanya vizuri kwa sasa na ngoma ya 'Mbele kwa mbele'  amesema inawezekana siku moja akajihusisha na fani ya sheria lakini mpaka aupate mongozo kutoka kwa Rais wa TLS, Fatma Karume.

Rapa Nay wa Mitego

Akizunguma kupitia www.eatv.tv, Nay amesema kwamba kwa sababu yeye siyo mtu anayependa siasa, anaamini mtu anapofahamu sheria anakuwa huru na  kujitambua.

Nay amesema kwamba sheria inaweza kuwa sehemu ya maisha yake endapo atapata miongozo hiyo kutoka kwa nguli huyo wa sheria nchini.

Mbali na kusiubiri miongozo ya Shangazi Karume amesema anapenda anachokifanya Mwanaharakati huyo ambaye ni shabiki wa muziki wake(Nay wa Mitego) jambo ambalo linazidi kumvutia kuipenda sheria.

"Napenda anachofanya Shangazi, nafurahi kusikia kwamba hata yeye ananikubali. Sipendi siasa lakini pia napenda sana vitu vinavyohusiana na sheria.

"Ukijua sheria unakuwa huru. Ningekuwa na uwezo ningejikita huko lakini siku nikipata bahati ya kukutana na shangazi Fatma Karume 'maybe' anaweza kunipa maneno mawili matatu nikajikuta naangalia huko zaidi," ameongeza Nay wa Mitego.

Mtazame hapa chini Nay akizungumza