Cicely Tyson
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na meneja wake Larry Thompson pamoja na familia haijaweka wazi chanzo cha kifo cha nguli huyo wa filamu duniani.
Tyson amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo medali ya Rais wa Marekani 'Presidential Medal of Freedom', mwaka 2016 ambayo alikabidhiwa na Rais wa Marekani wakati huo Barack Obama.
Cicely Tyson alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kupata nafasi ya kuigiza kama mhusika mkuu kwenye igizo la Television 'East Side/West Side' kwenye miaka 1960.
Tyson alishinda tuzo mbili za Emmys baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Autobiography of Miss Jane Pittman mwaka 1974.
Baadhi ya filamu zilizompa umaarufu ni "Sounder" (1972), "The Autobiography of Miss Jane Pittman" (1974), "Roots" (1977), "The Marva Collins Story" (1981), "The Women of Brewster Place" (1989), na "The Help" (2011).



