Ijumaa , 28th Oct , 2016

Msanii NIkki wa Pili ameitaka jamii kulikumbuka kundi la vijana ambao hawajafikia elimu ya chuo kikuu, lakini pia wapo kwenye janga la ukosefu wa ajira hapa nchini.

Nikki

 

Kwenye ukurasa wake wa instagram Nikki wa Pili ameandika ujumbe ambao unasema watu wengi wanapozungumzia suala la ukosefu wa ajira hukumbuka tu wale vijana waliohitimu chuo, huku wakisahau kundi kubwa la vijana ambao hawakufanikiwa kufika chuo kikuu lakini wapo mtaani, na kuwafanya wajione kama ni haki yao kutokuwa na ajira.

"Kumekuwa na midahalo na semina nyingi sasa kuhusu vijana na ajira....utawasikia viongozi, wasomi wakisema vijana wanamaliza chuo ajira hamna, ni kweli na tatizo litaendelea kuwa kubwa sana sana siku za usoni......lakini katika hii midahalo, harakati, matamshi kuna ubaguzi au uono mwembamba", aliandika Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili aliendelea kuandika ...."kuna vijana wengi wengi sana wanaomaliza primary na form 4, wamekuwapo miaka na miaka.....wengi katika hali mbaya.....mbona hili kundi ambalo ndio wengi karibun 80% hatulizungumzii .......kila siku ni wanaomaliza chuo hamna kazi.....hii inatoa justification kwa wasio fika chuo wajione wao wana haki ya kukosa kazi na wana haki ya kuikabili hali ngumu kimaisha....uono huu sio sahihi.....tuachane nao haraka", aliandika Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili amekuwa akizungumzia suala hilo mara kwa mara kama kijana aliyehitimu elimu ya juu, na kuwasaidia vijana wenzake kujifunza kupitia kwake na mtazamo wake juu ya masuala mbalimbali ya kijamii nje na masuala ya muziki anaoufanya.