Jumatano , 17th Jan , 2018

Msanii Nikki wa Pili aamua kufunguka juu ya kitendo cha wizara inayohusika na masuala ya sanaa kuwachukulia hatua wasanii kwa sababu zilizotajwa za kimaadili, na kusema kwamba suala hilo wasiliangalie kwa upande mmoja pekee.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Nikki wa Pili amesema kazi ya sanaa ina mapana yake, ambayo ukianza kuyachambua na kuangalia kutenda haki, hata wao wizara hawatakuwa salama kwa kutotimiza majukumu yao kwa wasanii.

Akiendelea kufafanua suala hilo, Nikki wa Pili amesema maadili ya msanii si tu kwenye muonekano wake, bali kuna mengine ambayo wao wizara wanatakiwa kuyasimamia kuhakikisha wote wawili wanakuwa kwenye mstari sahihi.

Msikilize hapa chini akifunguka