Ijumaa , 20th Mar , 2020

Mkongwe wa BongoFleva Dully Sykes, amesimulia tukio ambalo amekutana nalo kwenye maisha yake ya mahusiano, ambapo amesema alichanganyikiwa baada ya kuachwa na mama mtoto wake.

Msanii Dully Sykes

Dully Sykes amesema aliathirika baada ya kuachwa hali iliyompelekea kulala chini hadi leo hii na vitu vyote walivyonunua na mwanamke huyo, amevigawa kwa watu ili mradi asiendelee kumkumbuka.

"Mama wa mtoto wangu wa tatu aliniacha, kwa sababu tulikuwa tunaishi wote kwa muda mrefu bila kufunga ndoa, alivyoondoka sikuamini na iliniathiri hadi nilichanganyikiwa, meza ya vipodozi aliyokuwa anatumia nikaigawa, kitanda ambacho tulikuwa tunakilalia nikakigawa pia hadi leo nalala chini" ameeleza Dully Sykes.

Kwa urefu zaidi na mengine aliyoyazungumza tazama kwenye video hapa chini.