Kauli ya Mwana FA kuhusu video za Menina

Jumanne , 15th Oct , 2019

Neno 'Connection' limekuwa likiongelewa kila siku, hasa pale linapotokea tukio ambalo hushangaza watu na linalozungumzwa sana midomoni na kwenye mitandao ya kijamii.

Juzi kati zilizuka video na picha zisizo na maadili, zilizomuonesha Menina Tz akiwa mtupu, jambo ambalo lilipelekea akaitwa na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA), kwa lengo la kuzungumza naye ili kujua undani wa picha na video hizo.

EATV & EA Radio Digital, ilimpata msanii na mfanyabiashara Mwana Fa, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya BASATA kwa nia ya kulitolea ufafanuzi  suala hilo.

Sitaki swali hilo sijaziona kwanza hizo picha na sina 'connection'' amesema Mwana Fa.

Aidha Mwana Fa ameeleza  tukio lake la kukamilisha kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kusema.

Ilikuwa ngumu ila ni changamoto nzuri na kila mtanzania anatakiwa kuifanya katika maisha yake japo mara moja kwa sababu ina ugumu wake na ina ushujaa wake, kama umefanikiwa kuumaliza, kuna mahali ukitembea kila baada ya dakika 10 ilikuwa lazima ukae chini au unapanda kwa kutambaa” ameeleza Mwana Fa.