Jumamosi , 15th Feb , 2020

Mrembo Azzy Superstar amefunguka kusema hayupo kwenye mahusiano na mzungu mzee Wolf Rinner, kwa ajili ya kudanga au kutumia pesa zake japokuwa anahudumiwa na amepitwa uwezo wa kifedha na mzungu huyo.

[Picha ya Azzy Superstar akiwa na mumewe Wolf Rinner

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Azzy Superstar amesema kwa sasa yupo kwenye ndoa na Mzungu huyo huyo, mahusiano yao yalianza mwaka 2012, pia amezidiwa miaka 32.

"Sipo kwa ajili ya maslahi yangu binafsi huo ni mtazamo wa watu, halafu mimi sio mdangaji nilikuwa nafanya shughuli zangu ila huyu tu amekuja kuniongezea na ananihudumia kwa sababu ana uwezo wa kifedha zaidi yangu, kuna mambo mengine madogo madodgo nafanya kivyangu sihitaji msaada wake" ameeleza Azzy Superstar.

Aidha mrembo huyo ameendelea kusema,  "Kwenye umri amenizidi kwa miaka 32 na haikunipa shida yoyote kwa kutofautiana umri huo, kwenye mapenzi mimi naangalia upendo wa dhati kwanza, hata watu wangu wakaribu na wanaonifahamu walipoona nipo naye wakasema bora nikapumzike maana huko nyuma nimeshaumizwa sana" ameongeza.