'Nimesafiri nchi nyingi ila sipost' - Hamisa

Jumanne , 5th Nov , 2019

Msanii, Mrembo na Mjasiriamali kutoka Tanzania Hamisa Mobetto, amesema hana ushamba wa kusafiri kwenda sehemu za starehe, ikiwemo Dubai kama wafanyavyo mastaa wengine ambao wakienda sehemu hizo huwa wanapiga picha na kupost mitandaoni.

Akieleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital Hamisa Mobetto amesema, ameshasafiri karibia nchi nyingi zilizopo hapa duniani hivyo hana ushamba huo.

"Nilikuwa Dubai na nilishawahi kufika huko mara nyingi tu sio mara moja wala mara mbili, nimeshatembea katika nchi nyingi sana katika hii Dunia pia nina uwezo wa kujilipia mwenyewe tiketi nikaenda Dubai nikatumia pesa, kulala katika hoteli nzuri, nikala raha na nikarudi, kwa hiyo nipo vizuri" Hamisa Mobetto

"Sina ushamba wa kusafiri Dubai wala nchi yoyote ile sijawahi kuwa na ushamba, hakuna ubaya kila mtu anafanya kile kitu anachopenda yeye. wewe ukitaka kusafiri na unataka kupiga picha we piga picha tu una-enjoy, fanya kitu ambacho roho yako inapenda" ameongeza 

Hamisa Mobetto kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya uitwao sensema, aliyomshirikisha msanii Whozu, pia amechaguliwa kuwania tuzo za "Tanzania Consumer Choice Awards" katika kipengele cha Mwanamke aliyehamasisha zaidi katika upande wa biashara ndani ya mwaka 2019.