Ijumaa , 21st Feb , 2020

Msanii wa kike Nini amesema hajawahi kutoa ujauzito wa Nay wa Mitego na sasa hivi yupo tayari kubeba ujauzito wa mwanaume yeyote, ambaye atampatia kwa sababu kupata watoto ni baraka.

Picha ya Nini akiwa na Nay wa Mitego

Akiiambia EATV & EA Radio Digital, Nini amesema amekuwa akituhumiwa kutoa ujauzito wa Nay wa Mitego, tangu mwaka 2017 jambo ambalo sio la ukweli.

"Kwanini nitoe mimba, sina sababu ya kufanya hivyo, mimi bado mdogo halafu Nay ni baba mzuri kwa watoto wake namuona jinsi anavyowalea, hata nikisema niwe na mtoto najua atakuwa kwenye mikono salama, kuna watu kila siku wanataka watoto hawapati" amesema Nini.

"Ujauzito utakaokuja kwa mtu yeyote nitakuwa nayo tu, mtoto ni baraka hata sasa hivi nikipata mimba siwezi nikatoa, stori za kutoa ujauzito wa Nay wa Mitego nazisikia tangu mwaka 2017 kitu ambacho si kweli" ameongeza