Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nora achukua maamuzi mazito, ajivua rasmi

Jumatano , 19th Sep , 2018

Msanii wa filamu nchini, Nuru Nassoro maarufu kama Nora ametangaza rasmi kuachana na masuala ya sanaa ya uigizaji, huku akidai hata ikitokea amefariki hii leo atajisikia furaha kwa kuwa kazi iliyomleta duniani ameikamilisha.

Msanii Nora

Nora ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku akiwakosoa baadhi ya wasanii wa sasa wa filamu kuwa wamejawa na utandawazi, jambo ambalo linawapelekea kufanya mambo yasiyokuwa na maadili kwenye mitandao ili kusudi wapate kusifiwa, kujulikana na kupendwa.

"Nimeacha historia kwenye maisha yenu, kila mnapo nikumbuka kumbukumbu nzuri za furaha zinawajia kwenye vichwa vyenu, mpaka mnatamani enzi hizo zingekua zinarudi. Namshukuru MUNGU wangu sana kwa hili kwani ni kitu kizuri ukifanya kitu na watu wakakukumbuka kwa mazuri kiukweli ninapata furaha mnoo, ambayo haielezeki...

Japo najikuta najisikia vibaya wengine wanaposema walikua wanafukuzwa kwenye 'sitting room' za watu lakini ilibidi wakae madirishani na ikibidi wakate madirisha ya watu, wengine walikua wanakalishwa chini au inawabidi wafanye kazi ili jioni inapofika waangalie kipindi. Ninawatangazia rasmi nimeacha kuigiza.", ameandika Nora.

Pamoja na hayo, Nora ameendelea kwa kusema kuwa "mapenzi yenu yalikuwa sio ya kawaida wallah, hata nikifa leo kazi ilio nileta duniani ya kuwa burudisha na kuwafundisha nilifanya kwa ufasaha. Ama kweli enzi haziwezi kurudi, sasa hivi dunia imekua ya utandawazi watu wamekuwa wakilazimisha kupendwa, kusifiwa, kujulikana, inafikia wakati maadili hamna, mazoea ya kukaa pamoja kama familia na kuburudika na kujifunza".

Mbali na hilo, Nora amesema kuwa anajivunia kuwa msanii wa zama za zamani kuliko sasa, kwa kile alichokidai kwamba kizazi hiki kimeharibiwa na utandawazi katika kila kona.

"Nimeacha alama ambayo haitofutika daima niko hai au nimekufa, alama ambayo hata kwa Mungu ninacho cha kujitetea na akanielewa kwa kuwa siku lazimisha umaarufu ulikuja wenyewe, sikudanganyika na dunia bali niliishi kadri umri ulivyo nihitaji. Mara zote niliipigania heshima yangu kwenye kila kitu kama binadamu nilikosea lakini sio kwa makusudi eti ili niitawale dunia", amesisitiza Nora.

Nora alianza kujipatia umaarufu kwa jamii kupitia 'Kaole Sanaa Group', ambao walikuwa wanafanya maigizo yaliyokuwa yanayoeneshwa katika televisheni ya ITV.

Nora ni miongoni mwa wasanii waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya 'Dangerous Desire' ambayo alivaa uhusika wa mke wa Kanumba.

HABARI ZAIDI

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera