Jumanne , 30th Aug , 2016

Shindano la Dance100% la kusaka vipaji vya kucheza na kuendeshwa na EATV linatinga hatua ya nusu fainali Jumamosi Septemba 03, 2016 katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam.

Moja kati ya makundi yanayoshiriki katika shindano hilo

Akielezea maandalizi ya shindano hilo mratibu Bhoke Egna amesema maandalizi yanaendelea vizuri ambapo makundi 10 yatachuana ili kuweza kupatikana washindi watano ambao watapambana katika hatua ya nusu fainali ili mshindi aweze kupatikana.

“Maandalizi yanaendelea vizuri ambapo mashabiki wanakaribishwa sana na kutakuwa na zawadi kutoka kwa wadhamini wetu Coca- Cola pamoja na Vodacom , na washiriki wanaendelea vyema na maandalizi yao, hivyo mashabiki watarajie mambo mazuri” Amesema Bhoke.

Mshindi wa shindano la Dance100% atajinyakulia kitita cha milioni 7 ambapo ushindi wake utatokana na uwezo watakaouonesha kwa kuzingatia vigezo na masharti ya shindano hilo.

Ili kuweza kufahamu makundi yanavyopambana ili kuchuku ushindi wa Dance100% 2016, usikose kufuatilia EATV siku ya Jumapili saa moja jioni.

Tags: