.jpg?itok=vq6yq4vu×tamp=1577711598)
Officiall Nai akiwa na mpenzi wake Moni Centrozone.
Akipiga stori na Big Chawa, kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, Officiall Nai ameeleza jinsi alivyokutana na mpenzi wake huyo.
"Tupo kwenye mahusiano kwa mwaka wa nne sasa, nilikutana na Moni jijini Dodoma, wakati nilipoenda kupiga picha kwenye studio ndiyo nikamkuta huko, aliponitongoza nilichukua wiki moja ili kumjibu jibu lake na kumkubalia" amesema Officiall Nai.
Aidha ameendelea kusema hajaingia kufanya kazi ya u video vixen, labda kwa sababu alifeli shule, pia hawezi kushoot video ya laki tano kutokana na ukubwa wa jina lake kwa sasa na kwamba alianza kufanya shughuli hiyo mwaka 2017.
Nai pia amesema hayupo vizuri kwenye kuzungumza lugha ya Kiingereza.