Alhamisi , 25th Jun , 2015

Staa wa muziki Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa, mafanikio makubwa akitathmini alivyoweza kupenya kuingia 'mainstream', yametokana na kungundua mapema umuhimu wa kuwa na msaidizi na msimamizi katika kazi, akimpa shavu meneja wake wa siku zote Mubenga.

Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz amesema, tokea kufanyakazi kwake na Bendi na harakati za kusimama kama Solo Artist, alikwishapitia harakati nyingi na changamoto ambazo zilimfanya dhahiri kuamua kuanza safari hiyo moja kwa moja na meneja, kitu ambacho kimemfikisha alipo sasa akijivunia mafanikio makubwa aliyoyapata.