P Mawenge ataka kuzichapa ulingoni na Nikki Mbishi

Alhamisi , 14th Mei , 2020

Baada ya kupeana makavu "diss track" kwenye ngoma zao, P Mawenge amesema yupo tayari kuzichapa ulingoni na Nikki Mbishi kwa lengo la kutengeneza maslahi binafsi.

Wasanii wa HipHop kushoto ni P Mawenge kulia Nikki Mbishi

 

Wasanii hao wa HipHop wametrend sana kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuzungumziwa juu ya bifu lao ambalo kila mtu amemdiss mwenzake kwenye ngoma zao.

Akiieleza EATV & EA Radio Digital P Mawenge amesema "Nipo tayari na nipo vizuri, nafikiri watu wameshaanza kusogea juu ya jambo hilo na kuna harufu harufu fulani nimeanza kuisikia, ikikubalika itakuwa vizuri zaidi kwa sababu, mwisho wa siku tunafanya hivi ili kutafuta maslahi zaidi, nipo tayari na nanyoosha mtu tukienda raundi 5 zitatosha".

Aidha P Mawenge amesema bora Nikki Mbishi angemfuata au kumpigia simu kumwambia kama amekosea, kuliko kumchana kwenye wimbo kwamba baada ya kuomba collabo na msanii wa South Afrika Casper Nyovest, yeye kaomba picha.