Ijumaa , 10th Sep , 2021

Mpenzi wake Rayvanny, Paula ageuka kuwa video vixen kwenye wimbo mpya “Wanaweweseka” wa bosi huyo wa Next Level Music.

Picha ya Socialite Paula

Paula ametumika kama mwanamke aliyependezesha video ya wimbo huo mpya ikiwa ni mara yake ya kwanza kutokea kwenye kazi za muziki na huwenda akaingia katika anga za video vixens Bongo.

Kwa upande wa Chui hii itakuwa sio mara ya kwanza kufanya video na mpenzi wake, kwani alishafanya hivyo kwa Fahyma ambaye ametokea kwenye video zake tatu ambazo ni Kwetu, Natafuta Kiki na Siri.