Jumatatu , 14th Jan , 2019

Mchekeshaji Mc Pilipili ambaye hivi karibuni ali 'trend' kwenye mitandao ya kijamii kwa tukio la kutoa machozi pamoja na aina ya nguo aliyovaa siku ya kuchumbia, ametoa tamko lake kwa fundi aliyemshonea nguo hiyo iliyoleta taharuki mitandaoni,

Akizungumza na www.eatv.tv, Pilipili amesema alishona nguo hiyo kwa makusudi ili kutaka utofauti, na ndiye fundi anayemshonea nguo zake nyingi.

“'He is the best', anaweza kufanya nguo ambayo ikakustiri, lakini ikasababisha watu waizungumzie, mimi nimefurahi nimeipenda mno, hata valentine day nitavaa hii hii, lazima niwe na kitu ambacho ukikiona tu utazungumzia, ipo kama ninavyotaka mimi, amefanya vizuri”, amesema Mc Pilipili.

Nguo hiyo ya Mc Pilipili ilizua gumzo mtandaoni tangu siku ambayo alimvisha pete mchumba wake, Philomena Thadey maarufu 'Qute mena' huku akidhihakiwa kwa kufanana na mpishi, jambo ambalo mwenyewe amesema amelifurahia.