Jumanne , 4th Aug , 2020

Kutoka pande za Arusha msanii Bullranking amefunguka kuwa pisi za Arusha yaani wadada wa Mkoa huo wakiingia kwenye mahusiano huwa wanapenda kama vita na ukimzingua anaweza akakuhamisha nyumba.

Msanii Bullranking akiwa na mkewe

Bullranking amesema kama ukiamua kumpenda pisi ya Arusha, kubali kuacha mambo mengine na utulie naye, lakini ukizingua atakufanyia kitu mbaya.

"Binafsi sijakuwa na mahusiano na mtu mwingine kwa kipindi cha miaka 10 hadi tumekuja kuoana sijawahi kubadilisha pisi, ila ni kweli pisi za Arusha wanapendaga kama vita kama ukitaka kuwa na furaha kwenye mahusiano yako uwe umekubali kutulia na mwanamke mmoja, ndiyo vita itakuwa hakuna ila ukizingua utahama nyumba" amesema Bullranking.

Zaidi bonyeza hapo chini kutazama akizungumzia.