Jumamosi , 30th Jul , 2016

Kundi la P.O.D Crew ambalo limejitosa kwa mara ya kwanza katika ushiriki wa Dance100% limesema limeingia siyo tuu kushindana bali kuchukua ushindi wa mwaka huu 2016.

Kundi la P.O.D ambalo limeshiriki Dance100% kwa mara ya kwanza.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika kundi hilo mwenyekiti wa kikundi hicho Edd Bwigane amesema wameamua kujiunga na kufanya mzoezi kwa muda mrefu ili waonyeshe utofauti na namna walivyojipanga kwa kuzingatia ushindani uliopo.

‘’Sisi hatujaja kuonyesha tuu kwamba tupo, bali tumekamia kuchukua ushindi wa mwaka huu ili tuweze kuchukua hela zetu tukafanyie miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kujitanganza.

Aidha kwa upande wake Bwn Godfrey mmoja wa washiriki kwenye kundi hilo amesema hufanya mazoezi kwa muda wa masaa 7 kwa siku ili kujihakikishia kwamba nafasi yao ya kuingia mara ya kwanza na kuchukua kombe inawezekana.

‘’Huwa tunafanya mazoezi kwa muda wa saa 7 kwa siku ndiyo maana unaona kwenye kundi letu hakuna binti kwa kuwa wao kujituma katika mazoezi huishia kulalamika ndiyo maana tunapiga wenyewe ili tuweze kushinda’’ Amesema Godfrey.

Tags: