Jumanne , 19th Sep , 2023

Wimbo mpya wa Bahati Kenya "Huyu" umeondolewa YouTube kwa sababu ya Haki miliki ya Producer Genius Jini anayedai kuwa Bahati amecopy beat kutoka kwenye ngoma yake ya "Juu" aliyomshirikisha Jay Melody.

Picha ya Prod Genius Jini kushoto, kulia ni Bahati wa Kenya

Kupitia instagram ya Bahati ameshare picha inayoonesha ngoma hiyo haipo Youtube kwa sasa akiambatanisha na caption inayosomeka

"Shambulio lingine kutoka Tanzania, Genius Jini X66 ndio nani.? kuwa ubaya wake amefuta wimbo wangu wa 'Huyu' Youtube uliopo namba 2 Trending".

Kabla ya Prod Jini kushusha wimbo huo alimpa taarifa Bahati kama alitaka sound kama hiyo angemtafuta kumtengenezea kuliko kucopy idea yake.