Jumatano , 6th Apr , 2022

Q Chief  haimuingi akilini kabisa suala la Saraphina Tz kufananishwa na Vanessa Mdee kwenye muziki, Q Chief anasema Saraphina anafanya vizuri lakini nafasi ya Vanessa ipewe heshima yake sio wakufananishwa naye.

Picha ya msanii Q Chief

"Viatu vya mtu visivaliwe na mtu mwingine, yaani mnataka kumfananisha Saraphina na Vanessa Mdee kweli? anafanya vizuri kwenye game lakini tuheshimu kile tunachokiona kila siku" - Q Chief

Saraphina Tz amewahi kuweka wazi kuvutiwa na Vanessa Mdee kupitia mziki wake.