Jumamosi , 1st Feb , 2020

Msanii wa BonhoFleva Q - Chilla amesema moja ya vitu ambavyo anavutiwa navyo ni wasanii wenzake kumtambua kuwa yeye ni moja ya wakali wa muziki Tanzania, na kusema  hali hiyo inamuongezea heshima kubwa sana.

Msanii wa BongoFleva Q Chillah

Q Chillah ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha PlanetBongo cha East Africa Radio wakati akitambulisha ngoma yake mpya ya Utotoni.

"Mimi napenda sana ukifanya kitu ambacho mimi nakipendamimi , ndiyo maana huwa nafurahi sana kwa sababu unawaaminisha Mashabiki zako kuwa kuna kaka anayefanya muziki kama huu ninaoufanya." amesema Q - Chillah

Tazama video kamili hapo chini