Jumatatu , 16th Jun , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Rabadaba ameripotiwa kuwa katika ugomvi na meneja wa kundi jipya la 'Team No Sleep' Jeff Kiwa, chanzo cha ugomvi kikiwa ni mwanamke ambaye amefahamika kwa jina Lydia Jazmine.

Msanii wa Uganda Rabadada

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa, Jazmine ambaye ameingia mkataba wa kusimamiwa kazi zake na Jeff hivi karibuni, amekuwa na ukaribu wa kutatanisha na Rabadaba hasa baada ya kushirikiana katika kazi inayokwenda jina "I Need You", kitu ambacho kimemuudhi sana Jeff.

Kufuatia tukio hili, Rabadaba na Jeff wamekuwa mahasimu rasmi hasa kutokana Jazmine ambaye kutokana na hisia za meneja wake huyu, hafurahishwi na mahusiano ambayo Rabadaba ameanzisha naye.