
Kulia ni msanii Roma Mkatoliki, kushoto ni mchezaji Clatous Chama
Akifunguka hilo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Roma Mkatoliki ameandika kuwa
"Kuliko kuturusha rusha roho na kutuweka roho juu, tuambieni moja tujue na kujiandaa kisaikolojia Chama anaenda Uto au bado tupo naye".
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuna stori ambazo zinaendelea na zinasemakana kuwa huenda mchezaji huyo Raia wa Zambia akajiunga na mabingwa wa kihistoria hapa nchini Yanga SC.