Jumapili , 24th Jun , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ruby, amekanusha picha zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha akiwa amekonda mpaka mbavu kuonekana kuwa sio zake, huku akidai maishani mwake hajawahi kunenepa mpaka awe amekonda kiasi hicho.

Rubby ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' inayorushwa mubashara kupitia EATV kila siku ya Ijumaa baada ya kuzagaa picha hizo na kuzua gumzo na kupelekea baadhi ya watu kumuhusisha mwanadada huyo na utumiaji wa vilevi vikali pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi.

"Ile ni picha nasio Rubby halafu mnasema nimekonda kwani mlishawahi kuniona nimenenepa ?, haingii akilini kama vitu ambavyo vya negative wanavyoongea wakati mimi kazi ninafanya, ninaangalia mbele kwenye kazi zangu. Kazi yangu ndio inaongea lakini sio maneno ya watu. Mnaongelea mimi kuonekana mbavu zangu kwanini hamzungumzii kuonekana nina makalio makubwa", amesema Rubby.

Pamoja na hayo, Rubby ameendelea kwa kusema "ile picha ili kuwa imepigwa kwa pembeni angalieni video yangu niwaze ndio mtamuona Rubby nasio katika hizo picha, wawe wanaleta 'show' ili tunenepe".

Kwa upande mwingine, Rubby amesema kukaa kwake kimya kwa kipindi kirefu katika muziki alikuwa anataka kuja kivingine ili aweze kuwapa radha tofauti mashabiki zake wanaomfuatilia na kusikiliza kazi zake kila uchao.